WAKATI filamu nyingi za Tanzania zikiwa zinafanya vizuri kwenye masoko makubwa ya filamu ya nchini Ghana na Nigeria na Afrika kwa ujumla, msanii Irene Uwoya amedai kuwa kabla ya kumalizika kwa mwaka huu atafanya mchakato wa kutengeneza filamu na wasanii kadhaa wa nchini hizo ingawa bado anajipanga kwenye suala zima la fedha.
|
Uwoya akiwa location |
Akiongea na DarTalk alidai kuwa amekuwa akiweka ukaribu na kujenga urafiki na baadhi ya nyota wa filamu wa nchi hizo ili hata pale atakapoamua kuwashirikisha kwenye filamu zake iwe rahisi.
“Ni kweli tunahitaji kudumisha ukaribu kati ya Tanzania na nchi hizi mbili ambazo zinafanya filamu zinazoendana na sisi hivyo kwa upande wangu kama msanii ninayefanya vizuri nina hamu ya kucheza filamu moja na nyota wa nchi hizo, hivyo kwa sasa naweza kusema najipanga kwa hilo,”alidai.Labels: Filamu