Mathew Knowles: "Sitaki kuwa manager wa Beyonce, nataka kuwa baba yake".


Mathew Knowles, baba wa muimbaji mashuhuri Beyonce Knowles ameiambia TMZ kuwa alishaweka mambo sawa na mwanae muda mrefu kabla watu kupata taarifa zozote zile.

Mathew na Blush Music, kundi la muziki wa rap analolisimamia walikuwa wakila mitaa ya Beverly Hills na ndipo walipokutana na TMZ na kuweka wazi kuwa mahusiano yake na mwanae walishayasuluhisha hata kabla ya yeye na Blue Ivy kuonekana katika video mpya ya mwanadada Beyonce.