West Ham yamsajili Emmanuel Emenike kwa mkopo kutoka Fenerbahce


Klabu ya West Ham imethibitisha kumsajili kwa mkopo mnigeria, Emmanuel Emenike kutoka klabu ya Fenerbahce ya Uturuki.
Mshambuliaji huyo mwenye miaka 28, anaamini ataleta mabadiliko makubwa chini ya kocha Slaven Bilic ambaye amekuwa akimfahamu katika shughuli zake za ukocha katika nchi za Urusi na Uturuki.
"Nimeifahamu West Ham kama ni timu kubwa na nimekuwa nikiwaangalia pia. Nina furaha kubwa sana kuichezea klabu hii". Emenike aliiambia West Ham TV.