Tiwa Savage aweka wazi kwanini hakumpenda mume wake siku za mwanzo


Tiwa Savage hivi karibuni amefunguka na kuiambia media kuwa kabla ya kuingia katika uhusiano na mume wake Tunji Balogun, hakuwahi kumpenda kabisa kutokana na tabia yake ya kujisikia sana na kuongea chochote anachojisikia kuongea.

Akiongea na Pulse TV Tiwa Savage alisema mumewe huyo ambae anajulikana zaidi kwa jina la Tee Billz amebadilika mno na sio mtu ambaye alikuwa akimfahamu hapo mwanzo na ndio maana wakaweza kufikia hatua ya kuoana.

Huenda Tee aliamua kuweka pembeni tabia zake na kuamua kubadilika na ndicho kilichopelekea wawili hao kufikia hapo walipo licha ya kupata changamoto mbalimbali kutoka kwa familia ya nyota huyo wa Eminado.