Kanye West adai ana deni la $53m, amuomba Mark Zuckerberg amsaidie


Ilikuwa ni wikiendi busy kwa msanii Kanye West ambapo alikuwa akimalizia na kuiachia albamu yake mpya "The Life Of Pablo", albamu ambayo ameielezea kuwa ni moja katika ya albamu kali zaidi duniani.

Mara baada ya kuiachia albamu hiyo, West amekuja na kioja katika ukurasa wake wa Twitter ambapo amedai kuwa ana deni lipatalo dola milioni 53 za kimarekani na kuamua kumuomba mmiliki wa mtandao wa Facebook Mark Zuckerberg amsaidie kifedha.

Katika ukurasa wake Kanye aliandika,

I write this to you my brothers while still 53 million dollars in personal debt... Please pray we overcome... This is my true heart...
— KANYE WEST (@kanyewest) February 14, 2016

Mark Zuckerberg invest 1 billion dollars into Kanye West ideas
— KANYE WEST (@kanyewest) February 14, 2016

Rapper huyo aliwaomba mashabiki wake pia wamsaidie kumshawishi bilionea huyo ili akubali ombi lake na kumsaidia kiasi hicho cha fedha.