Wayne Rooney aonesha picha ya kwanza ya mtoto wake mpya wa kiume aitwaye Kit.


Mshambuliaji na nahodha wa klabu ya Manchester United, Wayne Rooney ameonesha picha ya baby boy wake aliyezaliwa jana kupitia ukurasa wake wa Twitter leo hii.

Rooney alitoa taarifa za kuzaliwa kwa mtoto huyo siku ya jana katika ukurasa wake wa Twitter masaa machache baada ya mpambano wa timu yake dhidi ya timu ya Southampton kuisha, match iliyopigwa katika uwanja wa Old Trafford.

Our gorgeous little boy arrived today. Kit Joseph Rooney. 8Ib 1oz. We are over the moon.
— Wayne Rooney (@WayneRooney) January 24, 2016



Akionesha furaha yake, Rooney alitumia mtandao wa Twitter tena kuonesha picha ya kwanza ya mtoto huyo leo.
Meeting Kit for the first time. Home time now 😀 pic.twitter.com/e4e2E6pOwk
— Wayne Rooney (@WayneRooney) January 25, 2016