(Photos) Jinsi Serengeti Fiesta 2014 ilivyofunika jijini Dar


Usiku wa kuamkia leo ulikuwa wa aina yake katika maeneo ya Leaders Club mara baada ya burudani kali kutoka kwa rapper wa Marekani T.I. 
Akionekana mchangafu jukwaani mwanamuziki huyo alitumbuiza ngoma zake kali za kitambo na zile mpya kutoka kwa album yake mpya 'Paperwork' ambayo itaachiwa Jumanne hii tarehe 21. 
T.I hata hivyo alichukua muda kuwaomba radhi mashabiki kwa kuchelewa kufika stejini na kuwalipa fadhila kwa performance hiyo ya aina yake katika usiku huo.
T.I alionekana pia kujibu watu wote walioongelea vibaya ziara yake ya kuja Africa na kusema yeye hajali watu wanaoizumgumzia vibaya Africa, na kuwachana kwa kibao cha 'Live Your Life'.
Kuelekea mwishoni, T.I alichukua picha ya pamoja na mashabiki "selfie" kama kuwashukuru kwa support walioionesha muda wote alivyokuwa akitumbuiza.
Licha ya T.I wasanii wengi kutoka Tanzania walitumbuiza pia akiwemo pia na Davido kutoka nchini Nigeria.
Tazama picha hapo chini:- 


Vanessa Mdee "Vee Money"

Ommy Dimpoz

Baadhi ya mashabiki waliohudhuria tamasha la Serengeti Fiesta

Banana Zorro

Young Killah

Waje kutoka Nigeria

Victoria Kimani

Rachel na wanenguaji wake 

Barnaba akitoa burudani ya aina yake

Mwanamuziki Shaa akikata mauno

Msanii kutoka Weusi Joh Makini nae akitumbuiza

Diamond Platnumz na Ney Wa Mitego wakitumbuiza pamoja

Msanii Davido kutoka nchini Nigeria akifanya yake stejini
Picha: Josephat Lukaza

Labels: ,