‘WEMA SEPETU’ ATOSWA KUCHEZA FILAMU NA ‘OMOTOLA’ WA NIGERIA


MSANII wa filamu bongo asiyeishiwa vituko Wema Sepetu, baada ya kutangaza kuwa anatarajia kwenda nchini Nigeria kwa ajili ya kucheza filamu moja na rafiki yake aliyewahi kumleta nchiniOmotola, sasa hana tena dili la kushiriki filamu moja na mwanadada huyo kwa kile kinachodaiwa kuwa tabia yake ya kujiskia sana.
Chanzo cha kuaminika kilichozungumza na mtandao wa DarTalk kwa sharti la kutotajwa jina, kilidai kuwa msanii huyo anashindwa kuwaeleza ukweli watanzania kuwa hawezi tena kukutana na msanii huyo, kwani anaona aibu kutokana mambo makubwa aliyoyafanya wakati alipomleta msanii huyo.

Wema akitoa burudani kwa mashabiki kwenye tamasha kubwa la Serengeti Fiesta morogoro

Chanzo hicho kiliendelea kusema kuwa Wema alikuwa na urafiki wa karibu sana na msanii huyo lakini kadri siku zinavyozidi kwenda ukaribu wao unapungua na kuna uwezekano mkubwa Omotolaakawa amebandilisha namba ya simu na hata email kwani haoni mazungumzo ya mara kwa mara kama ilivyokuwa awali.

“Kuna wakati alitangaza kuwa anataka kwenda kucheza filamu moja na msanii huyo lakini hizo habari sasa zimekufa na hakuna kinachoendelea kwani hawana mawasiliano yoyote na kitu kikubwa kilichotokea ni kwamba Omotola alimsomo Wema tabia yake na alihisi ni mtu wa kujisikia sana,”akilidai chanzo hicho.

Hata hivyo chanzo hicho kiliongeza kuwa kitendo kingine kilichomkatisha tamaa msanii huyo ni kutokana na skendo mbalimbali za Wema ambazo amekuwa akisoma kwenye mitandao kitu ambacho anaona wazi ni kwamba kinaweza kusababisha filamu ikauza upande mmoja wakati yeye anafanya kazi za kimataifa.

“Omotola alipokuja siyo kwamba alimpa uhakika wa moja kwa moja kuwa atamtumia kwenye filamu yake hapana, kitu ambacho alikifanya ni kuchukua baadhi ya filamu ambazo Wema amecheza na kuondoka nazo na alidai atakapolizika atamjulisha lakini hadi sasa kimya,” aliongeza.

DarTalk haikusita kumtafuta Wema na alipopigiwa simu namba yake hakuweza kupatikana huku rafiki yake huyo akidai kuwa mara nyingi huwa hawashi simu na ana namba zaidi ya tatu ambapo hata yeye mwenyewe wakati mwingine huwa hampati hewani.

Labels: