PINGU NA DESSO PAMOJA TENA



WAKALI muziki wa kizazi kipya Bongo Ramadhani Kalesela 'Pingu' na Deogratius Freddy 'Desso' ambao kitambo kidogo walitengana na kufanya kazi ya muziki wakiwa pande mbili tofauti kutokana na sababu za hapa na pale wamerudi kufanya kazi pamoja kama ilivyokuwa awali.

Akipiga stori na Teentz.com mapema leo Bosi wa Kruu ya 'Tip Top Connection', Bab Tale, ambaye ndiye amesimamia mpango mzima wa nyota hao kutoka upya wakiwa pamoja amearifu kuwa mara kadhaa alikuwa akipata maombi kutoka kwa mashabiki wa muziki wa kizazi kipya juu ya kuwaweka pamoja tena wakali hao hivyo akaona kuna haja ya kuheshimu mawazo ya mashabiki wake na kuamua kuweka kando tofauti zilizokupo na kuwatoa upya nyota hao kwenye ngoma mpya iliyopewa jina la 'Jicho Usimbanie'.…

Labels: